Habari Mseto

HUDUMA NAMBA: Ajenti matatani kwa kuitisha watu Sh300

May 16th, 2019 1 min read

Na PETER MBURU

HUKU Wakenya wakiwa katika pilkapilka za mwisho kujisajili Huduma Namba, imeibuka kuwa baadhi ya watu walioajiriwa kutoa huduma hizo wanatumia fursa ya watu wengi wanaojitokeza kupita kiasi, na kuitisha watu pesa ili kuwaharakishia.

Katika kanda ya video ambayo imekuwa ikizunguka kwenye mitandao, ajenti wa kusajili watu kuchukua Huduma Namba anaonekana akiitisha Sh300 kutoka kwa kila mtu, akisema mashine hazifanyi kazi na kuwa anataka kuendea mashine nyingine.

Aidha, mwanamke katika kanda hiyo anawahakikishia watakaolipa kuwa hawatapiga foleni kama wengine ili kuhudumiwa.

Lakini Wakenya wameghadhabishwa na tukio hilo na kukikashifu, wakitaka polisi kumkamata mhudumu huyo.