Huduma Namba: Waliodinda kujisajili kuadhibiwa

Huduma Namba: Waliodinda kujisajili kuadhibiwa

Na MARY WANGARI

WAKENYA ambao bado hawajajisajilisha kwa Huduma Namba huenda wakakosa huduma muhimu mswada uliowasilishwa na Serikali bungeni ukipitishwa kuwa sheria.

Mswada huo wa Huduma Bill 2019, uliowasilishwa na Waziri wa Usalama, Fred Matiang’i unadhamiria kuzuia utoaji wa baadhi ya huduma muhimu kwa Wakenya ambao hawatakuwa na kadi ya Huduma Namba kuanzia Desemba 2019.

Hatua hii ni mojawapo wa juhudi za serikali kuhakikisha kila Mkenya amejumuishwa katika Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Usajili (NIIMS).

Baadhi ya huduma ambazo hazitatolewa kwa Wakenya ambao hawana Huduma Namba ni pamoja na kuruhusiwa kuingiza watoto wao katika taasisi za umma za elimu, kusajilisha ndoa, kujiandikisha kama wapiga kura, na kuunganisha umeme katika nyumba zao.

Vilevile, ukiwa huna huduma namba utazuiwa kupata huduma ya afya kimataifa, kufungua akaunti ya benki au hata kusajilisha nambari ya rununu.

Hutaweza pia kupata idhini ya kununua au kuuza ardhi, kupata cheti cha usafiri, au hata kulipa ushuru

You can share this post!

Vibarua wa bandarini kuongezewa malipo kutoka Sh250 hadi...

Kina mama walevi watia wakazi hofu

adminleo