Huenda Guardiola akose kizibo cha Aguero

Huenda Guardiola akose kizibo cha Aguero

Na MASHIRIKA

MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola, alieleza kuwa bei ya wachezaji anaotamani huenda ikamkatisha tamaa na kumfanya kusalia na waliopo.

Shirika la British Media lilieleza kuwa Manchester City wamekuwa wakilenga Harry Kane wa Tottehnam au Earling Haalard wa Borrussia Dortmund kuziba nafasi ya straika huyo aliyeyoyomea Barcelona bila malipo.

Kane amenadiwa kwa zaidi ya Pauni 100 milioni(SH15 bilioni) naye Haalard akibadilishwa kwa kitita cha Sh22 bilioni.

Akizungumza na shirika moja la televisheni, Guardiola alikiri kuwa klabu yake inakabiliwa na hali ngumu ya kifedha kama klabu nyingine, hivyo huenda akatumia wachezaji alio nao.

“Hatuwezi kumudu gharama ya mastraika kwa sasa. Tunao Gabriel Jesus na Ferran Torres wanaoweza kuziba pengo hilo,” alisema.

Alisistiza kuwa uwezekano wa kununua mshambulizi msimu huu ni finyu sana, na huenda akalazimika kubadilisha mpangilio wa wachezaji kwa kutumia vinda alio nao.

Manchester City, ambao ndio mabingwa watetezi wataanza msimu dhidi ya Tottenham ugenini mnamo Agosti 15.

TAFSIRI NA: NDUNGI MAINGI

You can share this post!

Rais wa Haiti auawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake

Serikali yatoa Sh8.7 bilioni kusaidia familia maskini