Habari Mseto

Huenda wakazi wa Nairobi wanatumia unga ulioharibika

November 1st, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Huenda baadhi ya wakazi wa Nairobi wanatumia unga ulioharibika.

Hii ni baada ya maafisa wa polisi kuwafumania watu wawili Dandora wakipakia unga ulioharibika ndani ya mikoba mipya.

Kulingana na maafisa wa polisi, walivamia nyumba moja Siranga baada ya kudokezewa na umma na kupata washukiwa hao, Joyce Nyambura na Samuel Kamau, wakiwa na mtumba wa unga aina ya Exe, Dola na Golden Wheat.

Wachunguzi walisema unga huo uliharibika Julai 2018 na washukiwa hao walikuwa wakiutia ndani ya mikoba iliyo na siku mpya.

Mwezi jana, tani tano za nepi za kisasa zilizokuwa zimeharibika zilipatikana ndani ya bohari moja Mlolongo.

Washukiwa walipatikana wakipakia upya nepi hizo upya kwa lengo la kuficha siku za kutengenezwa na siku ya mwisho ambayo ilikuwa kati ya Januari na Mei 2017.