Huhitaji hela nyingi kununua chakula muhimu kwa afya yako

Huhitaji hela nyingi kununua chakula muhimu kwa afya yako

NA MARGARET MAINA

Mwmaina@ke.nationmedia.com

NUNUA vyakula vya kawaida visivyo ghali kama vile maharagwe na nafaka.

Vyakula hivi vina virutubisho zaidi na gharama yake ni nafuu kuliko vyakula ambavyo vimetengenezewa viwandani kama vile mkate mweupe, biskuti, na vyakula vilivyopakiwa kwenye makopo.

Kama unaishi kijijini, tafuta vyakula vya asili kama vile uyoga unaoliwa, mboga za majani za msituni na matunda, wanyama wadogo, au wadudu. Vyakula hivi mara nyingi huwa na virutubisho vingi, na havigharimu hela yoyote.

Fuga kuku kwa ajili ya mayai na nyama. Baadhi ya watu pia hujenga mabwawa madogo ya kufugia samaki watumike kama chakula nyumbani.

Panda chakula chako mwenyewe kwenye vyombo au bustanini.

Nunua chakula kila mara kwa wingi. Kununua chakula kidogo kidogo-kwa bei ya rejareja, huwa ghali zaidi kuliko kununua chakula kwa wingi na kwa bei ya jumla, chakula ambacho unaweza kutumia kwa muda mrefu zaidi.

Kama huwezi kumudu chakula kingi kwa wakati mmoja, unaweza kushirikiana na jirani yako au mwanafamilia, na baadaye kugawana gharama.

Epuka vyakula vya makopo yakiwemo maziwa yaliyoongezewa ladha. Baadhi ya vyakula hivi kwa kawaida huuzwa kwa ajili ya watoto wachanga na watoto wadogo. Vyakula hivi kwa kiasi fulani ni vya kukupotezea fedha. Maziwa ya kawaida ya mifugo au vyakula ambavyo vimepikwa vizuri na kupondwapondwa vina gharama nafuu zaidi na pia huleta afya zaidi kwa watoto kuliko “vyakula vya watoto wachanga” vilivyofungashwa viwandani au “maziwa ya watoto”.

Usitupe mchuzi wa maharagwe, nyama au mbogamboga ambao hutokea wakati wa kupika. Mchuzi huu umesheheni virutubisho na unaweza kuzuia anemia. Kunywa au tumia mchuzi huo kupika nafaka au vyakula vingine. Au pika na maji kidogo na kufunika chombo ili virutubisho vibaki ndani.

  • Tags

You can share this post!

AC Milan washinda taji la Serie A kwa mara ya kwanza baada...

Otieno afungia AIK bao kuibuka mchezaji bora wa mechi Uswidi

T L