Kimataifa

#HurricaneWilla yazua uharibifu Mexico

October 24th, 2018 1 min read

MASHIRIKA Na CECIL ODONGO

KIMBUNGA hatari almaarufu Hurricane Willa, Jumatano Oktoba 23 kilisababisha maporomoko ya ardhi eno la Pwani, Magharibi mwa Mexico kabla kiwango chake kupungua hadi dhoruba ya kawaida katika maeneo ya kati ya taifa hilo.

Hata hivyo hakuna maafa wala majeruhi yaliyoripotiwa huku kituo cha kitaifa cha kupambana na kimbunga hicho kikitoa onyo kwa raia kutotoka nje ili kuepuka visa vya maangamizi.

Villa kwanza iliathiri kisiwa cha Marias ambako kuna jela ingawa wizara ya usalama wa ndani ya Mexico haikufafanua iwapo iliwahamisha mahabusu 1000 au jinsi usalama wao ulivyohakikishiwa.

“Hatujapokea ripoti yoyote kuhusu uharibifu au vifo,” akasema mkuu wa idara ya huduma za dharura nchini humo Luis Felipe Puente katika kikao na wanahabari.

Kutokana na hatari iliyowakodolea macho wenyeji, zaidi ya watu 4,250 wakiwemo watalii waliokuwa likizoni katika ufuo huo walihamishwa hadi maeneo salama na kupata hifadhi ya muda katika mahema 58 yaliyowekwa na idara hiyo