Makala

Huzuni Kansa ikipokonya jamii ya waigizaji msanii Dida

Na FRIDAH OKACHI September 5th, 2024 1 min read

MWIGIZAJI wa vipindi vya televisheni Winnie Bwire Ndubi almaarufu Dida, ameaga dunia Septemba 5, 2024 alipokuwa akipokea matibabu Uturuki kutokana na ugonjwa wa Saratani.

Wasanii na Wakenya wameungana kumwomboleza mwigizaji huyo ambaye kwa miaka kadhaa amekuwa akipigana na Kansa.

Katika taarifa iliyotolewa na familia, ilithibitisha kuwa msanii huyo alifariki alipokuwa akipokea matibabu nje ya nchi.

“Kwa unyenyekevu na kukubaliana na mapenzi ya Mungu, tunatangaza Winfred Bwire Ndubi amefariki Septemba 5, 2024 kutokana na Saratani alipokuwa akipokea matibabu Uturuki. Tunashukuru kila mmoja kwa kutusaidia, maombi na ukarimu wenu,” ilisema taarifa hiyo.

Bwire alifahamika na wengi kwa uigizaji wake kwenye kupindi cha televisheni cha Sultana.

Alikuwa akiugua Saratani ya titi kwa kipindi cha miaka miwili.

Mnamo Desemba 2023, binti huyo, aliomba Wakenya kumsaidia kuchanga Sh7 milioni ili kutafuta matibabu nje ya nchi.