Huzuni moto ukiangamiza wanafunzi 16 Nyeri
WANAFUNZI 16 wamethibitishwa kufariki katika shule ya Hillside Endarasha Academy, Kieni, Nyeri, kufuatia mkasa wa moto uliotokea Alhamisi usiku, Septemba 5, 2024.
Msemaji wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi Resila Onyango amenukuliwa akisema kwamba wanafunzi wengine 14 walipata majeraha.
“Tuna wanafunzi 16 ambao wamefariki na 14 kujeruhiwa. Tunachunguza sababu na tutachukua hatua zinazohitajika,” alisema.
Moja ya mabweni ya wanafunzi hao iliteketea na kuangamiza wanafunzi 16, huku 15 wakichomeka kiasi cha kutotambulika na mmoja akifariki akikimbizwa hospitalini.
Habari zaidi zitafuata zinapochipuka