ICC yamruhusu wakili Gicheru kutumia ushahidi

ICC yamruhusu wakili Gicheru kutumia ushahidi

NA JOSEPH WANGUI

MAHAKAMA ya Kimataifa kuhusu Uhalifu (ICC) imemruhusu wakili Mkenya Paul Gicheru kutumia kijisehemu cha ushahidi wa upande wa mashtaka kujitetea katika kesi inayohusu kuingilia mashahidi.

Jaji Maria Samba jana Ijumaa alimruhusu Bw Gicheru kuwasilisha nakala 28 zinazosheheni ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka, wakati wa kesi yake inayohusu kuwahonga mashahidi katika kesi ya maovu ya kivita dhidi ya Naibu Rais William Ruto.

Timu yake ya mawakili wanaomwakilisha Mshtakiwa ikiongozwa na Bw Michael Karnavas, inaamini nakala hizo ni muhimu katika kumwondolea madai hayo.

Nakala hizo zinaambatana na mashahidi saba walioitwa kutoa ushahidi kortini na Afisi ya Mwendeshaji Mashtaka.

Bw Karnavas aliashiria kuwa Bw Gicheru hatafikishwa kwenye kizimba cha mashahidi kutoa ushahidi kama shahidi wa Mshtakiwa, badala yake atategemea kilichoandikwa kwenye nakala hizo.

“Korti hii inatambua nakala hizo kama zilizowasilishwa rasmi. Korti inaamuru Idara ya Usajili kuhakikisha data ya kielektoniki inaonyesha kuwa masuala yanayoibua utata yanatambuliwa kama yaliyowasilishwa rasmi Kortini,” alisema Jaji.

  • Tags

You can share this post!

Mtandao wa BrighterMonday wapendelewa zaidi na watafutaji...

Washukiwa 9 wa wizi wa mabavu watoroka seli za polisi Thika

T L