IEBC haina nia ya kuhujumu BBI – Chebukati

IEBC haina nia ya kuhujumu BBI – Chebukati

Na CHARLES WASONGA

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati amekana madai ya Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed kwamba tume inahujumu mchakato wa mageuzi ya Katiba kwa kuchelewesha ukaguzi wa sahihi za kuunga mkono mswada wa kufanikisha mpango huo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Bw Chebukati alisema kuwa shughuli hiyo ni hitaji la kikatiba wala sio shughuli iliyobuniwa na IEBC

“Tume ingependa kukana madai kuwa inahujumu mchakato wa marekebisho ya katiba kwa kuchelewesha shughuli ya ukaguzi wa sahihi za kuunga mkono mchakato wa marekebisho ya katiba. Shughuli hiyo ni sehemu ya wajibu wa IEBC kwa mujibu wa kipengele cha 257 cha Katiba na hivyo tume hii haiwezi kuhujumu mchakato huo,” Bw Chebukati akasema kwenye taarifa ilitumiwa kwa IEBC kwa vyombo vya habari Alhamisi.

Bw Mohammed ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa sekritariati ya BBI alitoa madai hayo Jumatano katika eneo la Burma, Nairobi, katika mkutano wa kuvumisha mchakato wa marekebisho ya Katiba kupitia BBI uliohudhuriwa na mchakato wa BBI.

Lakini katika taarifa yake Alhamisi Chebukati alisema kuwa makarani ambao tume hiyo iliwaajiri wanafanya kazi nzuri na wataikamilisha kwa wakati uliowekwa.

“Hatutakubali kushinikizwa na mtu au asasi yoyote,” akaeleza Bw Chebukati.

You can share this post!

SAMMY WAWERU: Visa vya askari kujiua na kuangamiza wenzao...

Jinsi ya kuandaa burger ya nyama ya ng’ombe