IEBC kuandaa kura mpya maeneo kadhaa

IEBC kuandaa kura mpya maeneo kadhaa

NA MARY WANGARI

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) hivi karibuni itaandaa chaguzi ndogo katika maeneobunge kadhaa, ikiwa bunge litaidhinisha uteuzi wa baadhi ya waliochaguliwa katika uchaguzi wa Agosti 9.

Hii ni baada yao kuteuliwa Jumanne na Rais William Ruto kuhudumu katika baraza la mawaziri.

Wakazi wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet watarudi kwenye debe kumchagua seneta mpya kufuatia kuteuliwa kwa Kipchumba Murkomen kuwa Waziri wa Barabara na Uchukuzi.

Wapiga kura wa eneobunge la Kandara katika Kaunti ya Murang’a nao watapiga kura tena kuchagua mbunge mwingine baada ya Alice Wahome kuteuliwa Waziri wa Maji na Usafi.

Katika eneobunge la Garissa Mjini, wakazi watachagua mbunge mpya kuchukua nafasi ya Aden Duale aliyetuliwa Waziri wa Ulinzi.

Wapiga kura hao watajiunga na wale wa Bungoma ambao pia watapiga kura kuchagua seneta mpya, kuchukua nafasi ya Moses Wetang’ula aliyechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Kitaifa.

  • Tags

You can share this post!

Kusikilizwa kwa kesi ya Kabuga kuanza kesho

Ruto ateua Koome kurithi Mutyambai, Kinoti ajiuzulu DCI

T L