IEBC yachapisha rasmi kwa gazeti la serikali Ruto ndiye rais mteule

IEBC yachapisha rasmi kwa gazeti la serikali Ruto ndiye rais mteule

NA CHARLES WASONGA

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imechapisha rasmi jina la Naibu Rais William Ruto katika gazeti rasmi la serikali, kama Rais Mteule.

Katika toleo la gazeti hilo la Agosti 16, 2022, mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati, alieleza kuwa Dkt Ruto alichaguliwa kihalali kwa mujibu wa mahitaji ya Katiba ya sasa.

Bw Chebukati alieleza kuwa Dkt Ruto na naibu rais mteule Rigathi Gachagua, sasa watakuwa na mamlaka ya kuendesha shughuli za serikali ya nchi hii, baada ya kuapishwa.

“William Ruto na Rigathi Gachagua wamechaguliwa kihalali kama Rais na Naibu Rais, mtawalia, wa Jamhuri ya Kenya. Hii ni baada ya kutimiza mahitaji yaliyoko kwenye kipengele cha 138 (4) cha Katiba wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne, Agosti 9, 2022,” Chebukati akasema.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi Uhuru alivyosaidia Ruto kuchaguliwa rais wa 5

Liverpool nguvu sawa na Crystal Palace katika EPL baada ya...

T L