Habari Mseto

Imam ashangaza kumlawiti mwanawe

November 2nd, 2018 1 min read

Na Charles Lwanga

Mwalimu wa madrasa anayedaiwa kumnajisi mwanawe wa kambo mwenye umri wa miaka tisa na baadaye akampatia Sh10 na kumuonya asiseme kwa mamake, amepatikana na hatia ya kosa hilo.

Hakimu Mwandamizi wa Malindi, Bi Silvia Wewa alimuhukumu Bw Omar Said Omar, ambaye ni imamu maarufu mjini Malindi, kwa kosa analodaiwa kulifanya mnamo Machi 23, 2016.

Bi Wewa alisema upande wa mashtaka umetoa ushahidi wa kutosha unaoashiria kuwa mshtakiwa alimlawiti mtoto huyo zaidi ya mara moja.