IMF kukopesha Kenya Sh262b kufufua uchumi

IMF kukopesha Kenya Sh262b kufufua uchumi

Na CHARLES WASONGA

MAAFISA wa Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) wanaozuru Kenya wametangaza kuwa shirika hilo litaipa Kenya mkopo wa Sh262.7 bilioni.

Katika taarifa kutoka ujumbe wa shirika hilo mkopo huo ambao utatolewa kwa kipindi cha miezi 38 ijayo utatumika kufadhili mipango ya kupambana na athari za Covid-19 kwa uchumi

“Makubaliano hayo hata hivyo bado yanasubiri kuchunguzwa na kuidhinishwa na Bodi ya IMF, katika wiki zijazo. Kando na kusaidia katika mpango wa kukabiliana na makali ya Covid-19 mkopo huo pia utasaidia kuweka msingi wa ukuaji wa kiuchumi katika miaka ijayo,” kiongoziwa ujumbe wa IMF Mary Goodman akasema.

Ujumbe huo umekuwa ukikutana na maafisa wa Kenya kwa njia ya mtandao kuanzia Desemba 9 hadi Desemba 17 mwaka jana. Hata hivyo, ulikamilishs utathmini wake mnamo Jumatatu, Februari 15, 2021.

Wanachama wa ujumbe huo walifanya mikutano na Waziri wa Fedha Ukur Yatani, Gavana wa Benki Kuu Nchini (CBK) Patrick Njoroge, Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua, miongoni mwa maafisa wengi wa ngazi ya juu katika serikali ya Kenya.

You can share this post!

Ngozi Okonjo-Iweala: Mwanamke na Mwafrika wa kwanza...

Mazishi yageuka rungu la kuchapa Ruto