Habari Mseto

Imwatok ashtakiwa kwa ulaghai

June 5th, 2020 1 min read

By RICHARD MUNGUTI

Kiongozi wa Wachache Bunge la Kaunti ya Nairobi Peter Imwatok alishtakiwa kwa kumtapeli mwanabiashara mmoja Sh2.1 milioni kwa kumdaganya kwamba angemuuzia shamba jijini.

Bw Imwatok aliyekuwa na vibali viwili vya kukamatwa kwa kosa lingine ambapo alistakiwa kwa kuwa na silaha kinyume na sheria katika korti ya Milimani.

Alikana madai hayo kwamba alimtapeli Bi Fresky Jepchichir Bett mwaka wa 2017 huku akijifanya kumuuzia shamba la nambari ya usajili 155/58..

Mwendesha mashtaka alisema kwamba Bw Imwatok, ambaye ni diwani wa Makongeni, alichukua pesa hizo kutoka kwa Bi Bett Frresky kati ya Februari 1 na Oktoba 31 mwaka wa 2017.

Wakili wake John Diro aliiomba korti kumwachilia diwani huyo kwa dhamana, akisema kwamba diwani huyo hawezi kutoroka.

“Mshukiwa hapa ni kiongozi wa wachache katika bunge la Nairobi na alijisalimisha mwenyewe kwa korti kama alivyo angizwa na polisi Jumatano,” alisema Bw Diro.

Bw Diro aliiambia mahakama kuwa mshukiwa ni mtu anayejulikana kwa hivyo atayafuata maagizo ya korti aliyowekewa..

Lakini hakimu aliuliza kwanini Bw Imwatok alikosa kuudhuria kikao cha korti cha shtaka lake la silaha. Bw Diro alieleza kwamba alikuwa mgonjwa na alikuwa na stakabathi za kuthitbitisha madai hayo.

Bw Imwatok aliachiliwa kwa thamana ya Sh200,000. Kesi hiyo itajajwa tena mwezi Julai .