Habari Mseto

Inasikitisha maafisa wa afya wanazidi kuambukizwa corona – Serikali

June 10th, 2020 1 min read

NA ANGELA OKETCH

Kutoa vifaa vya kuwakinga madaktari wasiambukizwe virusi vya corona na kuwepo kwa wagonjwa wasioonyesha dalili zozote za corona kumepelekea maafisa wengi wa afya kuambizwa virusi hivyo.

Waziri Msaidizi wa Afya Rashid Aman alisema kwamba inasitikisha kuona idadi ya maaafisa wa afya waoambukizwa virusi hivi ikiendelea kuongezeka ilhali walifunzwa kutumia vifaa hivyo.

“Itakuwa hatari kama idadi hiyo itaendelea kuongezeaka kwa sababu itahatarisha jamii na familia zao wenyewe. Tunahitaji mafunzo zaidi ya jinsi ya kutumia vifaaa hivyo,”alisema Dkt Aman.

Maafisa wa afya 81 tayari wameambukizwa virusi vya corona lakin hakuna hata mmoja amefariki.

Mombasa inanogoza kwa maafisa 41 ikifuatiwa na Nairobi na 31, Kiambu 4, Nyeri 3, Machakos, Kajiado na Laikipia zikirekodi kesi moja.