Ingwe wataka Namwamba afufue soka kuanzia mashinani

Ingwe wataka Namwamba afufue soka kuanzia mashinani

NA JOHN ASHIHUNDU

KLABU ya AFC Leopards imeungana na Wakenya wengine kumtaka Waziri mpya wa Michezo, Ababu Namwamba abadilishe uongozi wa kandanda nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa klabu hiyo Gilbert Andugu alisema ana matumaini makubwa kwa Waziri huyo mpya, ambaye ni miongoni mwa Wakenya wanaofahamu vyema mchezo huo kuanzia mashinani.

“Nampongeza rais kwa kumteua Namwamba kama Waziri wa Michezo, huku nikiwa na matumaini kwamba afisa huyo wa zamani wa Leopards ana uwezo wa kubadilisha uongozi wa mchezo huo kwa jumla. Ni jukumu kubwa, lakini tunapaswa kujitokeza kumuunga mkono.”

Namwamba atamrithi Amina Mohamed aliyepiga marufuku Shirikisho la Soka Kenya (FKF) kutokana na madai ya kufuja pesa za umma, hatua ambayo ilisababisha Kenya kufungiwa kucheza katika mashindano ya kimataifa tangu mwaka uliopita.

Andugu alitaka watakaopata majukumu ya kuusimamia mchezo huo waharakishe kufanya mazungmzo na Fifa ili Kenya irejeshwe katika mashindano ya kimataifa.

Namwamba ni miongoni mwa walioleta mabadiliko katika sheria za spoti nchini- 2013 Sports Act – kwa lengo la kulainisha mambo muhimu katika usimamzi wa michezo nchini.

  • Tags

You can share this post!

Malkia wa vita vya masumbwi Achieng’ kulimana na Melissa...

VALENTINE OBARA: Magavana wajitolee kugawia manaibu...

T L