Kimataifa

Iran yarusha makombora kuelekea Israel katika hatua inayozua wasiwasi wa vita

April 14th, 2024 1 min read

FATUMA BARIKI NA MASHIRIKA

SERIKALI ya Iran imeanzisha mashambulizi dhidi ya Israel, vyombo vya habari nchini Iran vimesema.

Ripoti ya tawi la jeshi la Iran, linalofahamika kama Iranian Revolutionary Force imesema kwamba mamia ya makombora na droni yamefyatuliwa kuelekea Israel, katika hatua inayochukuliwa kama kulipiza kisasi kutokana na kombora la Israel lililoua watu saba wakiwemo maafisa wawili wa Revolutionary Guards eneo la Damascus mapema mwezi huu.

Haya yanajiri wakati ambapo mshirika mkubwa wa Israel, Amerika amekuwa akihofia kuzuka kwa vita katika majuma kadhaa sasa, jambo lililopelekea Pentagon kutuma vikosi vya usalama eneo la Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo, ripoti za Pentagon zinasema kwamba Amerika inajaribu kunyaka makombora hayo ikisaidiana na ulinzi wa Israel kadri inavyowezekana huku Israel nayo ikijiandaa ‘kwa lolote’ kwa kufunga shule na kuandaa umma wake kwa vita vinavyohofiwa kuzuka wakati wowote.

Habari zaidi ni kadri zinavyojiri…..