Itumbi yuko na kesi ya kujibu katika dai kulikuwa na njama kumuua naibu wa Rais William Ruto

Itumbi yuko na kesi ya kujibu katika dai kulikuwa na njama kumuua naibu wa Rais William Ruto

By RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA mkurugenzi wa masuala ya dijitali katika Ikulu ya Nairobi Bw Dennis Itumbi atawekwa kizimbani kujitetea katika kesi ya kuchapisha habari za uwongo kwamba kulikuwa na  njama za kumuua Naibu wa Rais Dkt William Ruto.

Katika uamuzi aliotoa jana hakimu mkuu mahakama ya Milimani Martha Mutuku alisema kuna ushahidi wa kutosha kuwezesha korti kumwagiza Bw Itumbi ajitetee.Bw Itumbi ameshtakiwa pamoja na mwanaharakati Samwel Gateri Wanjiru kwa kusambaza habari hizo katika mitandao ya kijamii.

Bi Mutuku alisema, “Baada ya kuchambua ushahidi wote uliowasilishwa na upande wa mashtaka nimefikia uamuzi kuna ushahidi wa kutosha kuwezesha korti kuwaagiza washtakiwa wajitetee.”Bi Mutuku alitoa uamuzi huo kupitia mtandao.

Washtakiwa watafika kortini Septemba 23,2021 (leo) kutengewa siku ya kujitetea.Mabw Irumbi na Mr Gateri wanaotetewa na wakili Katwa Kigen wanakabiliwa na shtaka la kuchapisha barua kwenye mitandao ya kijamii iliyodai waziri mmoja alikuwa amepanga njama za kumuua Dkt Ruto.

Barua hiyo iliyochapishwa ilikuwa ya Mei 30 2019.Barua hiyo ilidai mkutano wa kupanga njama hiyo ulifanyika katika hoteli ya Lamada Nairobi.Washtakiwa hao walikanusha mashtaka dhidi yao ya kuchapisha habari ambazo zingelizua msukosuko miongoni mwa wananchi.

  • Tags

You can share this post!

Kashfa ya sukari yatibuka wakurugenzi wanne washtakiwa kwa...

Polisi wanne wanaoshtakiwa kwa mauaji wapatwa na Corona...