HabariKimataifa

IVF: Pacha wa baba tofauti wazaliwa kiteknolojia

January 29th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

HISTORIA imeundwa baada Pya mbinu za uzalishaji kwa kutumia teknolojia kuwezesha pacha wawili wa baba tofauti kuzaliwa huko Uingereza.

Alexandra na Calder, walizaliwa Jijini London, baada ya uja uzito kubebeshwa mama mwingine. Shughuli hiyo iligharimu takriban Sh2.5 milioni, kwa mbinu ya IVF (mimba bila kujamiiana).

Graeme ni babake Calder, naye Simon babake Alexandra. Watoto hao ni pacha kwa kuwa nusu ya chembechembe za uzalishaji zilitolewa kwa Graeme na nusu kwa Simon.

Hali hiyo iliwezesha pacha hao kuzaliwa, japo ni wa baba tofauti.

Simon ambaye ana miaka 43 alisema kuwa, “Inafurahisha kuwa Graeme name tumeweza kuzalisha mmoja wa pacha wetu sote.”

“Meg (mama aliyebeba ujauzito) alifanya kazi ya maana kwani iliashiria kuwa alibeba mimba ya wanaume wawili mara moja. Ni kwa sababu ya teknolojia ya IVF ndipo tumefanikisha hili,” akaongeza.

Alisema kuwa wamekuwa wakitaka kuwa na familia pamoja na Graeme, na kuwa walifurahi kufanikiwa kufanya hivyo mwishowe.

Hata hivyo, iliwabidi wawili hao kusafiri hadi Amerika kufanya kazi hiyo, kwani huko Uingereza bado hakuna teknolojia ya kufanya hivyo.

Walikutana na Meg, mama wa watoto wawili na aliye na miaka 32 kwenye mitandao ya kijamii.

Yai la mwanamke lilitolewa na mwanamke ambaye hakutambulishwa, ili kukamilisha mchakato wa uzalishaji, kisha Simon na Graece wakatoa ya kiume, walipokuwa Los Angeles.

Mayai yalizalishwa na miezi sita baadaye yakapandwa tumboni mwa ya Bi Meg.

“Hatukuelewana nani angekuwa baba ndipo tukaamua sote kuwa,” Simon naye akasema. “Hospitali ilisema kuwa ingewezekana kwa mayai kuzalishwa na nusu ya manii yangu na nusu ya Graeme.”

Meg alizaa baada ya wiki ya 36. “Ilikuwa furaha kuu maishani mwetu. Alexandra alitoka kwanza, kisha Calder dakika chache baadaye.”

Wiki saba baadaye, walirejea nyumbani kwao Uingereza.