Habari

Jacque Maribe na Jowie warudishwa rumande hadi Oktoba 24

October 17th, 2018 1 min read

NA RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA KUU Jumatano imeamuru mwanahabari Jacque Maribe na mchumba wake Joseph Iirungu (Jowie) warudishwe rumande hadi Oktoba 24, 2018 kesi dhidi yao itakapoendelea.

Jaji James Wakiaga alitahadharisha vyombo vya habari dhidi ya kuchapisha habari za ushahidi utakaohujummu haki za washtakiwa. Jaji huyo alisema atawachukulia hatua kali watakaokaidi agizo hilo.

Joseph Irungu (kulia) na Jacque Maribe (pili kutoka kulia) wakiwa kizimbani Oktoba 17, 2018 katika Mahakama Kuu ya Milimani, Nairobi. Picha/ Richard Munguti

Amesema wanahabari wamekuwa wakichapisha taarifa za ushahidi ambao haujatolewa mahakamani.

“Nimesoma katika magazeti jinsi mmoja wa washtakiwa amehusika na fedha za marehemu Monica Kimani,” Jaji Wakiaga amesema.

Jacque Maribe akumbatiana na mamaye mahakamani huku watu wakitizama. Picha/ Richard Munguti

Jacque Maribe na mchumba wake Bww Irungu wamekana kumuua Monica Wote na kuomba waachiliwe kwa dhamana.

Ombi lao litasikizwa hapo Oktoba 24 na sasa watasalia ndani kwa siku zingine saba.