Jaji afungulia wanasiasa wasio na digrii kuwania ugavana

Jaji afungulia wanasiasa wasio na digrii kuwania ugavana

Kupitia kwa wakili Harry Stephen Arunda, mpiga-kura huyo aliomba mahakama iharamishe sheria hiyo inayotaka wanaowania ugavana wawe wamehitimu kwa digrii.

Kesi hiyo ilifuatia nyingine ya Oktoba 2021 ambapo Jaji Mrima aliharamisha masharti kuwa MCA wawe na digrii ndipo wahitimu kuteuliwa na kuwania wadhifa huo.

Kufuatia uamuzi huo idadi ya wawaniaji wa kiti cha MCA iliongezeka katika uchaguzi mkuu uliopita.Awali Jaji Mumbi Ngugi wa Mahakama ya rufaa (akiwa jaji katika mahakama kuu) alisema wanaowania viti vya MCA na hata ubunge wasibaguliwe kwa masharti ya viwango vya elimu kwa vile watu wengi nchini walikosa kusoma kwa sababu ya ukosefu wa karo na sio eti kwamba hawawezi kuhitimu kimasomo.

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Tusije tukayazoea mauaji kama haya ya...

Hakikisho wafanyakazi 6,021 NMS wataajiriwa na serikali ya...

T L