Jaji alipanga njama za kumuua bwanyenye Tob Cohen, korti yaambiwa

Jaji alipanga njama za kumuua bwanyenye Tob Cohen, korti yaambiwa

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI wa uchunguzi wa Jinai (DCI) George Kinoti Jumatatu alifichua na kuweka wazi jinsi njama za kumuua bilionea Tob Cohen zilifanywa na mkewe marehemu Sarah Wairimu na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Sankale ole Kantai.

Katika afidaviti iliyowasilishwa mahakama kuu na naibu wa Inspekta Jenerali John Gachomo,imefichuliwa kuwa raia huyo wa Uholanzi mwenye asili ya Kiyaudi aliuawa siku mbili baada ya kugudua hisa katika kampuni yake ya Tob Limited zilikuwa zimeandikishwa kwa jina la mkewe (Wairimu) kisiri na kwa njia ya ufisadi.

Bw Gachomo ameanika jinsi Jaji ole Kantai na Bi Wairimu walivyofanya mikutano ya faragha na kupanga njama za kumuua Cohen.Familia ya marehemu Cohen ambaye maiti yake ilikutwa imetupwa ndani ya shimo la choo katika makazi yake.

Cohen alisemekana amesafiri ng’ambo kusaka matibabu.Jaji ole Sankale aliwashtaki DCI na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kwa kumtia nguvuni bila ushahidi kuonyesha jinsi alihusika na mauaji ya Cohen.

Katika taarifa hiyo ya kiapo akijibu madai katika kesi aliyoshtaki Jaji ole Sankale, Bw Gachomo, aliwasilisha ushahidi jinsi jaji huyo wa mahakama ya pili kwa ukuu nchini alivyohusika katika kupanga njama za kumuua bwanyenye huyo.

Bw Kinoti kupitia kwa Bw Gachomo ameeleza kwa undani jinsi jaji huyo alivyohusika katika utekelezaji wa mauaji ya Cohen.Pia DCI amefichua vile alipeleka faili ya uchunguzi wa Jaji ole Sankale kwa DPP isomwe kisha hatua ichukuliwe lakini akaondolewa lawama.

Wakili Danstan Omari anayewakilisha familia ya Cohen amesema kesi itawasilishwa ya kumtimua afisini Bw Haji kwa kumwachilia Jaji ole Sankale ilhali kulikuwa na ushahidi wa kuwezesha kumchukulia hatua jaji huyo.

Cohen aliuawa usiku wa Julai 19/20 2019 na maiti yake ikatupwa ndani ya shimo la choo. Bi Wairimu anayewakilishwa na Bw Philip Murgor amekanusha kumuua  mumewe.

Yuko nje kwa dhamana.

  • Tags

You can share this post!

Apatikana na hatia ya kumuua mwenye hoteli ya Ronalo

Chanjo ya corona ilivyo changamoto kwa wazee