HabariHabari Mseto

Jaji Odunga apelekwa Machakos majaji 17 wakihamishwa

February 14th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

JAJI mwenye tajriba ya juu, George Odunga , na anayesifika kwa maamuzi yake ya kihistoria amehamishwa hadi Mahakama Kuu ya Machakos kutoka Mahakama Kuu ya Milimani, Nairobi.

Jaji  Odunga aliyekuwa kinara wa kitengo cha kutetea haki katika mahakama kuu amebadilishana na Jaji Pauline Nyamweya.

Jaji  Odunga alishutumiwa kwa uamuzi wake kwamba maafisa wa kusimamia uchaguzi mkuu wa Oktoba 26, 2017 wa urais kwamba hawakuwa wameteuliwa kwa njia halali.

Uamuzi huo ulitisha kuzorotesha uchaguzi ambao washikadau wa chama cha Jubilee waliona kama unalenga kusitisha uchaguzi.

Jaji huyo alihamishwa katika zoezi lililowaathiri majaji wengine 17.

Jaji Richard Mwongo amepelekwa kusimamia mahakama kuu ya Naivasha huku Jaji Christine Meoli akipelekwa Mahakama ya Kiambu.

Jaji Joel Ngugi aliyekuwa Kiambu  amepelekwa Nakuru.

Wengine walioathiriwa ni Jaji Maureen Odero ametolewa Nakuru hadi Nairobi