Habari Mseto

Jaji Smokin Wanjala augua homa ya nguruwe akiwa India

February 26th, 2020 1 min read

Na BENSON MATHEKA

JAJI wa Mahakama ya Juu Smokin Wanjala, anaendelea kupata nafuu katika hospitali moja nchini India alikolazwa baada ya kuambukizwa homa ya nguruwe.

Jaji Mkuu David Maraga alisema Jaji Wanjala alikuwa India kuhudhuria kongamano la majaji alipoambukizwa homa hiyo hatari.

Kongamano hilo lilifanyika katika Mahakama ya Juu ya India.

“Jaji Smokin Wanjala ambaye amekuwa India kuhudhuria kongamani la majaji amelazwa hospitali na anaendelea kutibiwa homa ya nguruwe,” Bw Maraga alieleza kwenye taarifa.

Alisema majaji wengine sita wa Mahakama ya Juu ya India pia waliambukizwa homa hiyo.

Ingawa hakutoa maelezo zaidi, vyombo vya kimataifa vya habari viliropoti kuwa Jaji Wanjala alilazwa katika hospitali ya Apollo.

Habari ziisema Jaji Mkuu wa India Sharad Arvind Bobde aliagiza wafanyakazi wote wa Mahakama ya Juu ya India wapate chanjo dhidi ya homa hiyo.