Dondoo

Jamaa aamuru mke aache kazi alipoambiwa mdosi ni fisi sugu

March 1st, 2024 1 min read

KONOIN, BOMET

POLO wa hapa alimtaka mkewe aache kazi ya kuwa kijakazi katika boma jirani alipoambiwa kuwa mdosi wake hupenda warembo sana.

Inaarifiwa mume na mke walifurahi mdosi huyo alipompa mrembo kazi kwake kwa mshahara mzuri.

Hata hivyo, baada ya siku chache, polo aliingizwa baridi na marafikize hadi akaamua kubatilisha uamuzi.

“Mbona ulimwachia mrembo wako aingie pango la fisi? Umeweka asali yako katika hali hatari ya kurambwa,” mmoja wa marafiki wa jamaa alimwambia na kumtia tumbojoto.

Siku iliyofuata, kalameni alimwamuru mkewe asitie guu katika boma hilo akimwambia kuwa milango mingine ya heri itafunguka hivi karibuni.