JAMAL MUSIALA: Usimuone alivyo kinda, ana thamani ya Sh3.2 bilioni

JAMAL MUSIALA: Usimuone alivyo kinda, ana thamani ya Sh3.2 bilioni

Na GEOFFREY ANENE

Jamal Musiala ni mmoja wa makinda wanaovuma katika ulimwengu wa soka wakati huu. Kiungo huyo?mshambuliaji mwenye asili ya Ujerumani, Uingereza na Nigeria ni mali ya Bayern Munich.?Babaye ni Muingereza mwenye asili ya Nigeria naye mamaye ni Mjerumani.

Alianza kukuza talanta ya soka akiwa na umri wa miaka mitano katika akademia ya Lehnertz hadi mwaka?2010 wakati familia yake ilihamia nchini Uingereza alikolelewa kwa kipindi kikubwa cha utoto wake.

Alipowasili nchini Uingereza, Musiala alijiunga na Southampton akiendeleza talanta yake wakati uo huo?pia akisoma katika shule ya msingi ya Corpus Christi mjini Newport.

Alikuwa Southampton kwa miezi?minne kabla ya Chelsea kumnyakua mwaka mmoja tu baada ya kuwasili Uingereza.?Klabu ya Chelsea ilimpa ufadhili wa kukuza talanta yake.

Aliendelea kuimarika kwa haraka na kupewa?mechi yake ya kwanza kuchezea timu ya Chelsea ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 akiwa na umri?wa miaka 15, miezi miwili na siku 13.Wakati huo akivutia katika akademia ya Chelsea pia alikuwa na mchango wa kuaminika katika timu ya?taifa ya Uingereza.

Alichezea timu ya Uingereza ya Under-15 akiwa na umri wa miaka 13 na kuendelea?kupeperusha bendera ya nchi hiyo katika timu ya Uingereza ya Under-16.Alivalia jezi ya timu ya taifa ya Ujerumani ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16 mara mbili mwezi?Oktoba 2018.

Kisha, aliwajibikia timu ya taifa ya Uingereza ya Under-17, akiona lango katika michuano?yake miwili ya kwanza, na aliitwa kuchezea Uingereza hadi timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka?21.Musiala alijiunga na miamba hao wa Ujerumani kutoka Chelsea mnamo Julai 2019 akiwa na umri wa?miaka 16 pekee.

Mabadiliko hayo ya mazingira hayakumzuia kuendelea kupiga hatua katika soka yake. Alizoa takwimu za?kuridhisha ambapo alipata bao ama kusuka pasi iliyozalisha goli katika kila dakika 105 akichezea kikosi?cha Bayern cha wachezaji walio chini ya miaka 17 na kisha kupandishwa ngazi kusakatia ile ya Under-19.

Alijumuishwa katika kikosi cha pili cha timu ya watu wazima ya Bayern kabla ya mkurupuko wa virusi vya?corona mwezi Machi 2020.

Baada ya ligi kuanza tena, Musiala alicheza mechi yake ya kwanza ya soka ya malipo katika Ligi ya Daraja?ya Tatu akivalia jezi ya timu ya pili ya Bayern.

Aliifungia mabao mawili katika mechi yake ya pili.Alitoka kitini na kuchezea Bayern kwenye Ligi Kuu ya Bundesliga katika mechi ya raundi ya 33 dhidi ya?Freiburg na kuandikisha rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kabisa kuchezea timu hiyo.Alikuwa na miaka 17 wakati wa mchezo huo.

Alizoa rekodi nyingine alipofunga goli la mwisho katika ushindi wa Bayern dhidi ya Schalke wa 8-0 katika?siku ya kufungua msimu 2020-2021. Alikuwa na miaka 17 akifunga bao hilo na kufuta rekodi?ya Roque Santa Cruz aliyekuwa ameweka rekodi ya mfungaji mwenye umri mdogo kabisa wa Bayernakiwa na miaka 18.

Msimu huu, Musiala ametandazia Bayern michuano 16 na kucheka na nyavu mara?tatu ikiwemo dhidi ya Eintracht Frankfurt na RB Leipzig.Musiala, ambaye anaaminika kupokea mshahara wa Sh122,130 kila wiki (Sh6.3 milioni kila mwaka)?uwanjani Allianz Arena, anacheza kama nyota wa Tottenham Hotspur Dele Alli.

Juma lililopita, Musiala, ambaye thamani yake sokoni wakati huu ni Sh3.2 bilioni, alisherehekea kugonga?umri wa miaka 18 na kutangaza kuwa sasa hatakuwa mhamahamaji kati ya Uingereza na Ujerumani wala?kuchezea Super Eagles ya Nigeria.

Alichagua Ujerumani alikozaliwa. .na ambako anaishi na kula jasho ya? kazi yake.

You can share this post!

Man U washindwa kupiga Chelsea

Maelfu ya watahiniwa kukosa KCPE na KCSE