Habari Mseto

Jambazi apigwa risasi, mwenzake asakwa

September 1st, 2020 1 min read

By WAWERU WAIRIMU

Polisi wanatafuta jambazi katika kisa ambapo mwezake aliyekuwa anatengeneza bunduki alipigwa risasi Jumapili usiku eneo la Pepo Tumaini wadi ya Bulapesa.

Jambazi huyo aliyeuawa ni mmoja katika genge la majambazi ambalo limekuwa likihangaisha wafanyabiashara na kuwaibia usiku.

Mwezake alifanikiwa kuhepa wakati makabiliano hayo na polisi. Mwizi huyo ambaye hajulikani na hakuwa na stakabathi za kumtabulisha alikuwa anawashambulia wakazi dakika chache kabla ya saa tatu usiku.

Afisa wa polisi aliyekuwa anafanya msako aliitikia wito wa mwanaume mmoja ambaye kwa sasa anauguza majeraha  hospitalini na akampiga risasi jambazi huyo ambaye pia  alikuwa na bunduki la Ak-47 lililokuwa na risasi 23.

“Afisa aliyekuwa akifanya patro alipiga jambazi huyo risasi huku mwenzake akitoroka,” alisema kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Isiolo George Kariuki.

Mkuu huyo wa polisi alisema kwamba wanaendelea kutafuta jambazi huyo mwingine na kwamba wakazi wakipata habari zozote wasisite kupasha polisi.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA