Habari Mseto

Jambazi sugu aliyeachiliwa kimakosa asakwa

June 27th, 2020 1 min read

NA MACHARIA MWANGI

Wachunguzi wanatafuta jambazi mmoja aliyeachiliwa kimakosa kwa kupeana majina ya uongo.

Peter Kamau Ngige alikuwa amekamatwa kwa wizi wa mabavu lakini aliachiliwa kimakosa na korti kwani alikuwa na jina sawa na mfungwa mwingine aliyekamatwa kwa kosa la kuuza pombe haramu.

Katika kikao cha korti alijifanya kuwa mshatikiwa wa pombe haramu huku akiachiliwa bila maafisa wa gereza kujua.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Naivasha Samuel Waweru alithibitisha hayo na kusema wanendelea kumtafuta.

“Kuna maafisa wanendelea kumtafuta na tunatumaini kwamba atakamatwa hivi karibuni,” aliambia Taifa Leo.

Mshukiwa alikuwa na kesi kortini  iliyokuwa iamuliwe Juni 27, 2020 alipotumia kufanana kwa majina ili kuachiliwa.

Mpelelezi mmoja alimtambua mshukiwa huyo kama jambazi hatari anayehusika na wizi wa barabarani hasa mwaka wa 2018.

“Kabla tufanikiwe kumkamata aliwateka nyara madereva wa Matatu na kuwaibia wasafiri kwa kutumia bunduki,” alisema mchunguzi huyo.

Alikamatwa na polisi baada ya simu aliyoiba kufuatiliwa na kunaswa. Aliyenunua simu hiyo alisaidia polisi katika kumtafuta aliyemuuzia.

Bw Waweru alimtaja mshukiwa huyo kama hatari aliyehepa mitego ya polisi mara mingi kabla ya kukamatwa.

 

Tafsiri: Faustine Ngila