Jamhuri ya Czech yaponda Estonia bila huruma katika mechi ya kuwania tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia

Jamhuri ya Czech yaponda Estonia bila huruma katika mechi ya kuwania tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia

Na MASHIRIKA

KIUNGO Tomas Soucek wa West Ham United alipachika wavuni mabao matatu na kusaidia Jamhuri ya Czech kuwaponda Estonia 6-2 katika mechi ya Kundi E ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022.

Rauno Sappinen aliwaweka Estonia kifua mbele katika dakika ya 12 kabla ya Patrik Schick kusawazisha naye Antonin Barak kuwaweka Czech uongozini katika mechi hiyo iliyochezewa nchini Poland.

Soucek alifunga mabao mawili kabla ya mwisho wa kipindi cha kwanza na kufanya mambo kuwa 5-1 kufikia dakika ya 48.

Jakub Jankto aliwapachikia Czech goli la sita katika dakika ya Henri Anier kufunga goli la pili kwa upande wa Estonia kunako dakika ya 86.

Ufanisi huo ulikuwa mkubwa zaidi kwa Soucek ambaye awali, alikuwa amefunga magoli manne pekee kutokana na mechi 29 ndani ya jezi za Czech.

Chini ya kocha David Moyes, Soucek amewavunia West Ham jumla ya mabao tisa kutokana na mechi 32 za hadi kufikia sasa katika mapambano mbalimbali ya muhula huu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Dkt Ruto asema ni kufa kupona Harambee Stars ikikwaana na...

Mpango wa MKU kujenga hospitali ya kisasa