Habari Mseto

Jamii yahimizwa kukoma kuficha watu walemavu

May 28th, 2018 1 min read

Na OSCAR KAKAI

ZAIDI ya walemavu 6,000 katika kaunti ya Pokot Magharibi hawajasajiliwa kutokana na mila na utamaduni wa kuficha walemavu.

Mshirikishi wa shirika la Rehab Mission, Bw Tom Mulati alisema hali hiyo inawazuia walemavu kupata elimu na misaada.

“Tunawaomba wakazi kufichua wale ambao wamefichwa ili waweze kupata msaada. Wengi huchukuliwa kama laana na wengine kutelekezwa,” alisema Bw Mulati.

Akiongea mjini Kapenguria, mshirikishi huyo alitoa wito kwa walemavu kuomba zabuni kutoka kwa serikali ya kaunti

“Wengi hawajitokezi ama wanakuja kama wamechelewa. Tunaomba wakazi kuweka wazi wale ambao wamefichwa,” akasema.