Jamii yalalamika kutatizwa na operesheni ya usalama Boni

Jamii yalalamika kutatizwa na operesheni ya usalama Boni

Na KALUME KAZUNGU

WAKAZI wanaopakana na msitu wa Boni katika Kaunti ya Lamu, wamelalamikia mahangaiko ambayo wamepitia miaka sita tangu Kikosi cha Ulinzi Kenya (KDF) kilipoanzisha operesheni ya kukabiliana na magaidi msituni humo.

Jamii zinazoishi maeneo hayo zimeitaka serikali kuchukua hatua ili wasaidiwe kurudia hali yao ya kawaida ya maisha, jinsi ilivyokuwa kabla operesheni hiyo ya ‘Linda Boni’ kuanza mnamo 2015.Katika maeneo hayo, ni watoto wa chekechea hadi darasa la nne pekee ambao wanaendeleza masomo, ikilinganishwa na takriban watoto 400 wanaostahili kuwa shuleni.

Wanafunzi wa darasa la tano hadi nane husafirishwa kwa ndege za jeshi au mashua hadi shule ya bweni ya Mokowe Arid Zone iliyoko eneobunge la Lamu Magharibi, ambapo ni umbali wa karibu kilomita 320 kutoka msitu wa Boni, kila muhula.

“Kila shule zinapofunguliwa, wakati mwingine tunaambiwa ndege hakuna. Kukodisha boti hadi Mokowe ni ghali. Watoto wengi hapa wameacha shule kutokana na hii hali,” akasema mzee wa Nyumba Kumi katika kijiji cha Kiangwe, Bw Abdalla Wakati.

Hata hivyo, walieleza matumaini kuwa shule mpya iliyozinduliwa na KDF eneo la Mokowe mnamo Septemba, huenda ikatatua tatizo hilo.Shughuli zao za kujitafutia riziki pia zimeathiriwa mno huku huduma muhimu kama vile elimu na afya zikipata pigo kubwa.

Jamii ya Waboni tangu jadi imekuwa ikitegemea urinaji wa asali kujikimu kimaisha. Lakini tangu operesheni ya kufurusha magaidi msituni ilipoanza, wamezuiwa kuingia humo.Jaribio lao kuendeleza ufugaji wa nyuki katika maboma yao sasa limepata pigo, baada ya nyuki kutoroka sababu ya kiangazi cha muda mrefu.

“Nyuki hutengeneza asali pahali ambapo pana maji na maua. Jamii ya Waboni inatambulika kwa kusambaza asali kwa wingi ndani na nje ya Kaunti ya Lamu. Inasikitisha kwamba biashara hiyo sasa haiwezekani,” akaeleza Bw Abatika Ali.

Mwanajamii mwingine Bi Khadija Musa alilalama kuwa wameguzwa ombaomba kutegemea misaada ya serikali na wahisani, ilhali wao ni watu wenye bidii ya kujichumia kitega uchumi.“Shughuli zetu zote za riziki zimeathirika tangu serikali itangaze marufuku ya kuingia msituni miaka kadhaa iliyopita.

Tumekuwa wa kutegemea misaada sasa; misaada yenyewe haiji siku zote. Tunaumia!” alihoji Bi Musa.Katika sekta ya afya, zahanati tatu zilizotegemewa – Milimani, Basuba na Mangai – zimefungwa baada ya wahudumu kuondoka wakihofia usalama wao kufuatia mashambulizi ya kigaidi.

ambapo baadhi ya vituo vya afya vilivamiwa na dawa kuibwa.Wahudumu karibu wote wa afya waliokuwa wakifanya kazi kwenye vituo hivyo vya afya walitoroka maeneo hayo kwa kuhofia usalama wao kufuatia mashambulio ya kigaidi ambapo baadhi ya vituo vya afya vilivamiwa na dawa kuibwa.

“Tumechoka kusafirisha wagonjwa wetu kutoka Boni hadi mjini Lamu ambako ni mbali kutafuta huduma za hospitali,” akasema Diwani wa Wadi ya Basuba, Bw Deko Barissa.

You can share this post!

Gavana apongeza hatua za kufufua sekta ya korosho

Raia mwingine wa kigeni apatikana amefariki ndani ya meli...

T L