Habari Mseto

Jamii za mpaka wa Nandi na Kakamega zatakiwa kuishi kwa amani

June 5th, 2020 1 min read

NA SHABAN MAKOKHA

Wanasiasa kutoka eneo la magharibi wameanzisha kampeni kukuza kuwepo kwa ushirikiano kati ya jamii zinazoishi katika mpaka wa Nandi na Kakamega.

Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa, Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya, Bw Noah Nekesa na Bw Fred Gumo waliwahimizia watu wa jamii ya Kabras waishi kwa amani na majirani zao wa Nandi.

Bw Wekesa alisema kwamba Waluhya na Wanandi wameishi kwa amani na kuoana jambo ambalo halifai kuharibiwa na tofauti ndogo za kifamilia.

“Kutoka niwe Gavana mwaka wa 2013 hii ni mara ya tano nashuhudia mvutano katika mpaka wa Nandi na Kakamega. Tumeweka mikutano mingi ya maelewano lakini bado vita huendelea,”alisema Bw Oparanya.

Aliiomba serikali kuu kuingilia kati ili kutafuta suluhu. Waziri Wamalwa alisema kwamba wataendelea kufanya mikutano ya maridhiano.