Japhet Koome ateuliwa awe Inspekta Jenerali wa polisi, Mutyambai akistaafu

Japhet Koome ateuliwa awe Inspekta Jenerali wa polisi, Mutyambai akistaafu

NA SAMMY WAWERU

RAIS William Ruto amemteua Bw Japhet Koome kuwa Inspekta Jenerali Mkuu mpya wa Polisi (IG).

Dkt Ruto ametoa tangazo hilo Jumanne baada ya kustaafu kwa IG anayeondoka, Bw Hillary Mutyambai.

Rais amesema hali ya afya ya afisa huyo mkuu ilimlazimu kuchukua likizo, ambayo imemshinikiza kustaafu.

Majuma kadha yaliyopita, Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi (DIG) kutoka kitengo cha askari tawala, Noor Gabow alitwaa kwa muda nafasi ya Bw Mutyambai baada ya kutangaza kulazwa hospitalini kupata matibabu.

“Japheth Koome ni Kamanda wa Chuo cha Mafunzo ya Askari, Kiganjo,” Dkt Ruto akasema.

Tangazo la kuteuliwa kwa Bw Koome, alilitoa akihutubu Ikulu ya Nairobi katika hafla ambayo pia alizindua baraza la mawaziri la serikali yake.

IG huyo atapigwa msasa na kamati ya usalama bungeni, ili kuidhinishwa rasmi.

Ruto pia alitangaza kujiuzulu kwa Mkurugenzi Mkuu Idara ya Uchunguzi wa Jinai na Uhalifu (DCI), Bw George Kinoti.

Rais aidha ameitaka Idara ya Polisi (NPS) kutangaza wazi nafasi hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Maafisa watano wa polisi washtakiwa kwa kumuua mahabusu

Naibu Gavana ataka wanaomponda Achani wanyakwe

T L