Habari Mseto

Jela la Nairobi lafungwa

October 6th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Jela la Nairobi limefungwa kutokana na kuzuka kwa virusi vya corona huku wafungwa 35 wakiwa wameambukizwa virusi hivvyo, serikali ilitangaza Jumanne.

“Hakuna yeyote anaruhusiwa kutembea kwenye jela hilo kwani mamlaka ya jela hilo likijaribu liwezavyo kupunguza msambo wa virusi vya corona,” alisema katibu msaindizi Dkt Rashid Aman Jumanne.

Dkt Aman alisema kwamba asilinia 55 ya visa vilivyoripotiwa Nairobi vilikuwa vinatoka rumande. Maafisa wa afya walisema kwamba jela hilo haitapokea wafungwa kuanzia Jumatano.

Wizara ya Afya ilitangaza visa vipya vya corona 137 Jumanne huku idadi ya maambukizi ikifikia 39,586.

Wizara hiyo pia iliripoti vifo nane Zaidi huku idadi ya vifo ikifikia 743 na waliopona wakifikia 26,331.