Michezo

Jepkosgei na Mutiso kutetea ubingwa Gifu Seiryu Half Marathon

April 8th, 2018 2 min read

Na GEOFFREY ANENE

MSHIKILIZI wa rekodi ya dunia ya mbio za mseto za kilomita 21, Joyciline Jepkosgei na Mkenya mwenzake Alexander Mutiso watatetea mataji yao ya Gifu Seiryu Half Marathon nchini Japan hapo Aprili 22, 2018.

Baadhi ya washindani wakubwa wa Jepkosgei, ambaye pia anashikilia rekodi ya Gifu Seiryu ya saa 1:07:44, ni mshindi wa mwaka 2016 Eunice Kirwa kutoka Bahrain, na Wakenya Valary Jemeli na Joy Kemuma.

Baada ya kuwasili kutoka mjini Valencia nchini Uhispania alikoshiriki Riadha za Nusu-Marathon Duniani mwezi Februari, Jepkosgei alisema mojawapo ya malengo yake ya mwaka 2018 ni kuvunja rekodi ya dunia.

Hakutangaza mashindano atakayotumia kufanya hivyo kwa hivyo kwa sasa chochote chawezekana katika mashindano yoyote ya kilomita 21 atakayoshiriki yakiwemo Gifu.

Mutiso atakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Wakenya wakiwemo James Mwangi, James Rungaru na Nicholas Kosimbei, Mganda Moses Kurong na wenyeji Japan.

Orodha wa wakimbiaji walioingia Gifu Seiryu Half:

Wanawake

Joyciline Jepkosgei (Kenya) saa 1:04:51 (Valencia 2017)

Eunice Chumba (Bahrain) 1:06:11 (Copenhagen 2017)

Valary Jemeli (Kenya) 1:07:50 (Prague 2017)

Joy Kemuma (Kenya) 1:09:02 (Venlo 2018)

Karolina Nadolska (Poland) 1:09:54 (Posnan 2017)

Ftaw Zeray (Ethiopia) 1:10:31 (Marugame 2018)

Mao Kiyota (Japan) 1:10:31 (Valencia 2015)

Sayo Nomura (Japan) 1:11:22 (Sanyo 2015)

Sinead Diver (Australia) 1:11:40 (Valencia 2018)

Yuko Aoki (Japan) 1:12:14 (Sanyo 2017)

Yuko Watanabe (Japan) 1:13:08 (Sanyo 2015)

Yuko Mizuguchi (Japan) 1:13:13 (Sendai 2017)

Marie Imada (Japan) 1:13:54 (Marugame 2018)

Andrea Seccafien (Canada)

Sayaka Takarada (Japan)

 

Wanaume

James Mwangi (Kenya) dakika 59:07 (Copenhagen 2016)

James Rungaru (Kenya) 59:37 (Den Haag 2018)

Moses Kurong (Uganda) 59:50 (Copenhagen 2017)

Nicholas Kosimbei (Kenya) saa 1:00:21 (Lisbon 2018)

Alexander Mutiso (Kenya) 1:00:31 (Lisbon 2018)

Edward Waweru (Kenya) 1:00:31 (Marugame 2018)

Macharia Ndirangu (Kenya) 1:00:57 (Gifu Seiryu 2017)

Joel Mwaura (Kenya) 1:00:59 (Marugame 2017)

Patrick Muendo (Kenya) 1:01:51 (Gifu Seiryu 2016)

Yohei Suzuki (Japan) 1:01:53 (Marugame 2018)

Daniel Muiva Kitonyi (Kenya) 1:02:05 (Nat’l Corp. Half 2017)

Ser-Od Bat-Ochir (Mongolia) 1:02:08 (Marugame 2016)

Michael Githae (Kenya) 1:02:27 (Gifu Seiryu 2015)

Takuya Fukatsu (Japan) 1:02:29 (Osaka 2018)

Shun Sakuraoka (Japan) 1:02:44 (Ageo 2016)

Desmond Mokgobu (Afrika Kusini) 1:02:48 (Port Elizabeth 2015)

Suehiro Ishikawa (Japan) 1:02:49 (Marugame 2016)

Shintaro Miwa (Japan) 1:02:59 (Marugame 2018)

Hayato Sonoda (Japan) 1:03:00 (Marugame 2016)

Yuki Kawauchi (Japan) 1:03:11 (Ageo 2015)

Yuichi Okutani (Japan) 1:03:21 (Osaka 2017)

Yuya Ito (Japan) 1:03:22 (Hakodate 2015)

Yasuyuki Nakamura (Japan) 1:03:32 (Ageo 2017)

Dishon Maina (Kenya) 1:03:35 (Gifu Seiryu 2016)

Kenta Matsumoto (Japan) 1:03:38 (Gifu Seiryu 2015)

Yuichiro Ogawa (Japan) 1:03:44 (Marugame 2016)

Taiga Ito (Japan) 1:03:52 (Gifu Seiryu 2015)

Shota Hattori (Japan) 1:05:13 (Sendai 2016)

Ezekiel Jafary (Tanzania) 1:06:19 (Moshi 2015)