Jeremiah Kioni akubali kushindwa katika eneobunge la Ndaragwa

Jeremiah Kioni akubali kushindwa katika eneobunge la Ndaragwa

NA WANDERI KAMAU

MBUNGE anayeondoka wa eneobunge la Ndaragwa Jeremiah Kioni amekubali kulemewa na mgombea wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) George Gachagua, baada ya matokeo ya awali yasiyo rasmi kuonyesha pengo kubwa kati ya wanasiasa hao wawili.

Bw Gachagua amepata ushindi mkubwa dhidi ya mbunge huyo wa sasa katika karibu nusu ya vituo 124 ambavyo vilikuwa vimeshatuma matokeo.

“Kwa wakazi wa Ndaragwa, ninawapongeza kwa kunipa fursa ya kuwa mbunge wenu. Ninayakubali matokeo haya bila kinyongo. Pongezi kwako Mheshimiwa George Gachagua kwa kuchaguliwa. Ninawashukuru wote waliofanya kazi chini yangu, timu yangu ya kampeni na jamii pana ya Ndaragwa. Mungu Awabariki wakazi wa Ndaragwa na awajalie mengi mazuri,” amesema Bw Kioni.

  • Tags

You can share this post!

Alexis Sanchez ayoyomea Ufaransa kuchezea Olympique...

CECIL ODONGO: Wakenya wadumishe amani wakisubiri matokeo ya...

T L