Habari za Kitaifa

Jeshi lakanusha kuhusika katika tukio la kupiga, kuvamiwa kwa kituo cha polisi

April 18th, 2024 1 min read

NA MWANDISHI WETU

JESHI la Kenya limekanusha kuhusika kwa wanajeshi wake katika tukio la kupigwa kwa polisi na kuvamiwa kwa kituo cha polisi eneo la Lodwar Jumatano.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Alhamisi, Jeshi linasema kwamba limefedheheshwa na video, picha na maandishi mitandaoni kwamba wanajeshi wake walikamatwa na kutupwa katika seli za Kituo cha Polisi cha Lodwar Jumatano Aprili 17, 2024.

“Madai ya kuzuiliwa kwa wanajeshi yanafedhehesha, kudunisha na yananuia kuzua taharuki na ni jambo tunalochukulia kwa uzito mkubwa kwa sababu linahujumu ushirikiano baina ya vikosi,” ikasema taarifa hiyo.

Linashikilia kwamba kufikia sasa, uchunguzi wao umebaini kwamba wanajeshi wao hawakuhusika kupiga afisa wa polisi wala kuvamia kituo cha polisi kama ilivyodaiwa.

Jeshi sasa limesema linafanya uchunguzi wa kina kubaini haswa kilichojiri na kuchukua hatua zinazofaa.