Jicho Pevu aponea shambulio la risasi

Jicho Pevu aponea shambulio la risasi

NA FARHIYA HUSSEIN

MBUNGE wa Nyali, Bw Mohamed Ali, amenusurika baada ya watu wasiojulikana kufyatua risasi katika afisi zake.

Kufuatia tukio hilo lililotokea Jumanne, mbunge huyo alisema anaamini maisha yake yako hatarini kwa vile si mara ya kwanza yeye kuvamiwa.

“Kuna dalili tosha kwamba mtu au watu waliohusika na jaribio hili la kutaka maisha yangu hawajachoka,” akasema mbunge huyo kwenye taarifa.

Kulingana naye, hii ni mara ya tano jaribio aina hii kutokea kwake, akihofia maisha yake na familia yake.

Akithibitisha kisa hicho, Naibu Mkuu wa Polisi wa eneo la Nyali, Bw Dafalla Ibrahim alisema uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha shambulio hilo.

Shimo linaloaminika kusababishwa na risasi lilionekana kwenye dirisha la afisi ya mbunge huyo.

Duru zilisema maganda ya risasi yaliyopatikana kwenye eneo la tukio yametumwa Nairobi kwa uchunguzi wa kina.

  • Tags

You can share this post!

Raila atangaza Machi 20 kuwa siku ya mapumziko

Faida za kiafya za oregano

T L