JIJUE DADA: ‘Coil’ isipokaa vizuri utahisi uchungu mwingi!

JIJUE DADA: ‘Coil’ isipokaa vizuri utahisi uchungu mwingi!

NA PAULINE ONGAJI

KUNA baadhi ya wanawake ambao hukumbwa na tatizo la kitanzi au ukipenda IUD (Intra-Uterine Device) au koili kusonga na kusababisha maumivu makali na kuvuja damu nyingi.

Ni suala ambalo ili kuangalia mkao wa kifaa hiki, unapaswa kukaguliwa na mwanajinakolojia ambapo pia utapigwa picha ya ultrasound scan.

Ikiwa kwa kweli kifaa hiki kimesonga, chaweza kurejeshwa katika sehemu inayofaa au hata kuondolewa.

Mwanajinakolojia aidha, atakukagua kubaini iwapo una matatizo mengine yanayosababisha maumivu ya tumbo kama vile shida ya mfumo wa uzazi au wa kupitisha mkojo, au hata tatizo la utumbo.

Kuna wale ambao wakati huu huu pengine huenda wakaanza kuhisi maumivu ya wayo na kudhani kwamba tatizo hili limechangia.

Lakini ukweli ni kwamba mara nyingi shida hii huwa tofauti. Yaweza kuwa kutokana na kuvimba kwa tishu nyepesi katika sehemu hii.

Kumbuka kwamba maumivu haya ya wayo yaweza sababishwa na uzani mzito, au ikiwa una mazoea ya kusimama au kutembea kwa muda mrefu, au ikiwa wayo zako ni bapa au endapo utao wa mguu wako uko juu (high foot arch).

Kuvalia viatu visivyohimili vyema tao za miguu yako pia huchangia tatizo hili.

Ili kukabiliana na tatizo hili, fanya mazoea ya kujinyosha na kukanda miguu yako kabla ya kuondoka kitandani. Valia viatu vinavyohimili vyema tao za miguu yako na vilivyo na visigino tulivu au vilivyoinuka kidogo.

Aidha, dawa za kukabiliana na maumivu zitapunguza uchungu na uvimbe kwenye sehemu hii.

You can share this post!

TIBA NA TABIBU: Wasiwasi huku idadi ndogo ikijitokeza...

CHARLES WASONGA: Uteuzi tata wa Igathe huenda ukamkosesha...

T L