JIJUE DADA: Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi na kwa muda mrefu

JIJUE DADA: Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi na kwa muda mrefu

NA PAULINE ONGAJI

MABINTI wengi hukumbwa na hali inayofahamika kama Menometrorrhagia/menorrhagia pasipo kujua.

Pengine wewe ni mmoja wa wanaouliza hii ni nini? Hili ni tatizo linalohusika na hedhi ambapo mhusika hupoteza damu nyingi.

Kuna mambo kadha wa kadha yanayosababisha hali hii ikiwa ni pamoja na:

•Kutokuwa na usawa wa kihomoni: Kutokuwa na usawa wa homoni za estrogen halikadhalika homoni zingine zinazohusika na uzazi hupelekea kuota kuliko kawaida kwa ukuta wa fuko la uzazi, na hivyo kumpelekea mhusika kuvuja damu kupita kiasi wakati wa hedhi.

•Matatizo ya ovari: Upungufu wa homoni za progesterone wakati wa hedhi hupunguza usawa wa homoni mwilini na kusababisha hali hii.

•‘Fibroids’: Uvimbe huu unaoota katika fuko la uzazi la mwanamke hupelekea kuvuja damu kusiko kwa kawaida.

•‘Polyps’: Huu ni uvimbe unaoota katika ukuta wa ndani wa fuko la uzazi.

•‘Adenomyosis’: Wakati mwingine endometrium (ukuta wa makamasi ndani ya fuko la uzazi) huingia ndani ya misuli ya fuko la uzazi na hivyo kusababisha kuvuja damu kusiko kwa kawaida.

•Matumizi ya aina kadha za mbinu za kupanga uzazi zinazohusisha kuingiza kwa kifaa katika njia ya uzazi (IUDP).

•Matatizo ya ujauzito kama vile mimba kuharibika.

•Kansa: Aina mbalimbali za kansa kama vile ya ovari, fuko la uzazi, ukuta wa fuko la uzazi na njia ya uzazi zaweza leta shida hii.

•Historia ya matatizo ya damu katika familia.

•Aina fulani za dawa.

Ishara za hali hii

•Kuvuja damu kupita kawaida wakati wa hedhi huku mhusika akitokwa na damu wakati usio wa hedhi pia.

•Kuvuja damu chini ya siku 21 au zaidi ya siku 35 kabla ya siku za hedhi.

•Kuzidi kutokwa na hedhi kwa zaidi ya siku saba.

•Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo hasa wakati wa hedhi.

•Mwathiriwa huonyesha ishara za maradhi ya anemia kutokana na kupoteza damu nyingi.

  • Tags

You can share this post!

MUME KIGONGO: ‘Magonjwa ya wanawake’ ambayo...

Shikanda ashukuru Ingwe kumwamini

T L