Jinsi ya kuandaa minofu ya kuku iliyopakwa siagi

Jinsi ya kuandaa minofu ya kuku iliyopakwa siagi

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

· kuku kilo 1

· juisi ya limau

· chumvi kijiko 1

· pilipili ya unga vijiko 3

· tangawizi iliyosagwa kijiko 1

· majani ya bay 3

· mdalasini uliosagwa kijiko 1

· siagi vijiko 3

· vitunguu maji 2

· vitunguu saumu vijiko 5

· giligilani vijiko 2

· nyanya ya kopo vijiko 2

· maziwa mgando vijiko 2

· mafuta ya kupikia

· chumvi

Maelekezo

Andaa nyama ya kuku kwa kuisafishe vizuri.

Chukua pilipili manga, tangawizi, majani ya bay, mdalasini, maziwa mgando, vitunguu maji, vitunguu saumu, giligilani, na nyanya ya kopo. Chukua blenda weka hivyo vitu vyote kisha saga na uhakikishe vimelainika kabisa na viungo vimechanganyikana vizuri.

Chukua kuku ukate vipande.

Chukua bakuli kubwa, changanya na juisi ya limau, weka na chumvi.

Mimina mafuta ya kupikia kwenye kuku, changanya vizuri mpaka uone mafuta yameenea vizuri.

Chukua ile rojo halafu mwagia kwenye kuku, kisha changanya. Ukimaliza weka kwenye jokofu kwa muda wa saa moja halafu utoe minofu ya kuku ili upake siagi. Changanya kisha rudisha tena kwenye jokofu usiku mzima.

Toa na ukaange na viungo upendavyo. Unaweza kuoka au unaweza kuchoma.

Dakika 25 zikifika toa minofu hiyo kwa sababu itakuwa imeiva.

Pakua na chochote ukipendacho na ufurahie.

  • Tags

You can share this post!

SHAIRI: Ndoto yangu yazimika

Stima, Rangers zagawanya pointi debi ya Mombasa