Jinsi ya kuandaa wali wa mayai

Jinsi ya kuandaa wali wa mayai

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

 • wali uliopikwa vikombe 4
 • mayai matano
 • manjano robo kijiko cha chai
 • mafuta ya kupikia vijiko viwili
 • kitunguu maji kimoja kilichokatwakatwa
 • pilipili mboga ya rangi nyekundu iliyokatwakatwa nusu kikombe
 • njegere nusu kikombe
 • chumvi kiasi
 • sukari robo kijiko cha chai
 • pilipili robo kijiko cha chai
 • vitunguu vya majani viwili vilivyokatwakatwa

Maelekezo

Chukua wali – mchele ambao umeshaupika –  uchambue vizuri kisha utie katika sahani au sinia pana. Acha upoe kabisa.

Vunja mayai matatu katika bakuli moja, kisha vunja mayai mengine mawili pamoja na maji vijiko viwili vya chakula, tia manjano kisha ziweke pembeni bakuli zako zote mbili.

Baada ya hapo, weka kikaangio au sufuria yako mekoni. Weka moto wa kiasi kisha tia mafuta ya kupikia kiasi ya vijiko viwili vya chakula. Yakipata moto, weka mayai matatu uliyoyavunja, bila viungo. Yavurugevuruge. Epua weka pembeni.

Weka tena chombo mekoni katika moto mkali, tia mafuta kijiko kimoja cha chakula. Yakipata moto, weka vitunguu na pilipili mboga kisha kaanga kwa dakika mbili.

Tia wali wako kisha geuzageuza vizuri ili wali upate moto vizuri.

Mimina mayai mabichi uliyoyakoroga na viungo juu ya wali wako kisha kaanga kwa dakika moja hadi mayai yaenee vizuri katika wali.

Chukua njegere, weka kisha koroga bila kuachia kwa muda wa dakika moja, nyunyuzia chumvi, (na sukari ukipenda) na pilipili juu ya wali wako kisha koroga vizuri kuchanganya.

Ukiona wali ni mkavu sana, mimina maji ya uvuguvugu kidogo au supu.

Baada ya hapo, acha uive vizuri kisha weka mezani tayari kuliwa.

You can share this post!

ULIMBWENDE: Jinsi ya kutunza vidole na kucha

Matatu zaendelea na huduma licha ya uvumi wa mgomo