Makala

Jinsi ya kupika maharagwe yaliyotiwa manjano

June 25th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa kupika: Dakika 30

Walaji: 5

Vinavyohitajika

• kilo ½ maharagwe yaliyochemshwa

• vijiko 2 vya mafuta ya kupikia

• kijiko 1 cha binzari ya manjano

• kitunguu maji 1

• nyanya 1

• kijiko 1 cha nyanya ya kopo

• tui la nazi kikombe 1

• chumvi

Maelekezo

Weka nyanya na kitunguu kwenye blenda na utengeneze rojo.

Chemsha mafuta ya kupikia kwenye sufuria katika moto wa chini kiasi. Ongeza rojo ya nyanya na kitunguu, binzari ya manjano na uchanganye vizuri, kisha funika mpaka iive.

Ongeza maharagwe, tui la nazi na nyanya ya kopo. Funika tena; acha chakula kichemke mpaka sosi iwe nzito.

Sasa mimina au nyunyuzia chumvi kiasi wastani.

Maharagwe yako sasa yako tayari. Yapakue ama na wali, chapati, au chochote ukipendacho na ufurahie.