Jinsi ya kupika samaki kwa wali au sima

Jinsi ya kupika samaki kwa wali au sima

Na DIANA MUTHEU

dmutheu@ke.nationmedia.com

Muda: dakika 45

Vinavyohitajika kupika samaki

Samaki 1

Tangawizi (kipande kimoja cha wastani)

Mafuta ya kupika

Karai ya kukaranga samaki/sufuria

Vinavyohitajika kupika mchuzi wa nyanya

Nyanya 4

Vitunguu 2

Biringanya 1 (toa ngozi ya juu)

Pilipili hoho ½

Kitunguu saumu Kipande 1

Dania

Mafuta ya kupikia vijiko 2

Chumvi

Sufuria na kifuniko yake.

Jinsi ya kuandaa samaki

Saga tangawizi kisha uipake katika samaki yako iliyo safi, kisha uiweke kando kwa muda wa dakika kumi.

Tumbukiza samaki yako katika mafuta yaliyochemka, ikiiva epua na uiweke kando hadi mafuto yote yadondoke.

Jinsi ya kuandaa supu ya nyanya

Katakata viungo vyako (Nyanya, vitunguu, hoho, biringanya na kitunguu saumu) kisha uviweke vyote ndani ya sufuria.

Ongeza mafuta vijiko 2 na chumvi ya kutosha (pia waeza kuongeza viungo vingine unavyopenda)

Funika sufuria yako kisha uwache viungo hivyo viive kwa muda wa dakika tano kwa moto wa wastani hadi viunde mchuzi. Ukipenda mchuzi wako uwe mwepesi sana, ongeza maji kiasi.

Ongeza dania na katika mchuzi huo, koroga kisha epua.

Pakua na ufurahie.

Waweza kuandaa mboga hii kwa ugali au wali.

You can share this post!

Masaibu yamsukuma kuishi kwa nyumba ya wazee

Undeni mfumo wa ugavi wa fedha wa kuunganisha taifa -Ruto