Makala

Jinsi ya kutengeneza shake ya vanilla na maziwa

December 3rd, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Wanywaji: 2

Vinavyohitajika

• ndizi mbivu 2

• maziwa glasi 2

• sukari kijiko 1

• vanilla kijiko 1

• custard kijiko 1 (ingawa sio lazima)

• vipande vya barafu

Maelekezo

Osha ndizi zikiwa na maganda yake vizuri. Menya ndizi na ukate kisha weka kwenye jagi la blenda.

Mimina maziwa kwenye ndizi. Weka sukari, custard na vanilla.

Malizia kwa kuweka vipande vya barafu.

Chukua jagi weka kwenye blenda kisha saga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika kadhaa.

Rudia kusaga kwa mara ya pili; ikisagika vizuri mimina kwenye glasi.

Furahia kinywaji chako.

Angazio

Kama huna barafu saga na maziwa ya baridi.

Ukipenda ya baridi sana weka kwenye jokovu.

Kama mchanganyiko ni mzito sana mimina maji kiasi kidogo.

Sio lazima kuweka sukari.