Habari MsetoSiasa

Jipe moyo, Moses Kuria amwambia Jacque Maribe mahakamani

October 17th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MBUNGE wa Gatundu kusini Bw Moses Kuria alifika mahakamani Jumatano kufuatilia kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa mpeperushaji wa habari za televisheni katika kituo cha Citizen Jacque Maribe.

Bw Kuria alimsalimia Bi Maribe na kumwambia ajipe moyo. Alimshauri ajikakamue kwa vile sheria itachukua mkondo wake na hatimaye atajua hatima yake.

Bali na Bw Kuria, aliyekuwa mkurugenzi wa masuala ya dijitali Bw Dennis Itumbi alifika mahakamani mapema  na kuzugumza na Bi Maribe kwa muda mrefu.

Hatimaye Bw Itumbi alijadiliana na wakili Katwa Kigen anayemwakilisha wa Bi Maribe katika kesi hiyo ya mauaji.

Bi Maribe aliwasilisha ushahidi kwa njia ya afidaviti huku kiongozi wa mashtaka Bi Catherine Mwaniki akiomba muda wa kujibu.

Mahakama iliwataka mawakili Samson Nyaberi na Cliff Ombeta wawasilishe maombi yao kwa muda unaofaa ndipo Bi Mwaniki apate fursa ya kujibu ushahidi wa mchumba wa Maribe, Joseph Kuria Irungu almaarufu Jowie.

Kesi itaendelea Oktoba 24, 2018.