Habari Mseto

Jitokezeni mpimwe corona, Muturi awahimiza wabunge

July 1st, 2020 1 min read

By SAMWEL OWINO
Spika Justin Muturi aliwahimiza wabunge wajitolee wapimwe virusi vya corona kabla ya kikao cha bunge kuanza.

Bw Muturi aliambia wabunge hao kuhakikisha wamepimwa kabla ya kuenda kutangamana na majimbo yao..

“Hakikisha kwamba mmeweka umbali wa mita moja unusu pia,” spika aliwaambia wabunge.

Hayo yalikuja baada ya mbunge wa Wajir Kaskazini Ahmed Abdisalan kutolewa nje baada ya kuigia kwenye bunge bila barakoa

“Wabunge hawafi kuvunja mikakati iliyowekwa na wizara na afya ya kudhibiti virusi vya corona .Mbunge huo anpaswakutolea nje,”aliagiza spika.

Spika Muruti alidhibitisha kwamba wabunge wawili wana virusi vya corona.Lakini za kuainika zinasema kwamba wabunge sita wanavirusi vya corona.

Majina ya hao wabunge yatabaki siri. Aliongeza kwamba wabunge ni wanadamu na wanweza pata virusi hivyo.

Bw Muturi alisema wamehakikisha kwamba wabunge wao wako salama.

“Kuna uvumi wa vyombo vya habari kwamba wabunge ambao wamepata virusi vya corona ni wawili. Nimewapa habari hiyo ili kuhakikishia umma ukweli,”alisema.

Tafsiri: Faustine Ngila