JKF yatenga Sh22.2 milioni kwa wanafunzi kutoka familia za kipato cha chini

JKF yatenga Sh22.2 milioni kwa wanafunzi kutoka familia za kipato cha chini

Na KENYA NEWS AGENCY

WAKFU wa Jomo Kenyatta (JKF) mwaka huu umetenga Sh22.2 milioni ili kuyashughulikia masomo ya wanafunzi kutoka familia za kipato cha chini katika shule za upili.

Pesa hizo hazitatumika kufadhili masomo hayo pekee bali pia kununulia vitabu na vifaa vingine vya masomo kwa wanafunzi maskini walioteuliwa kutoka kaunti zote 47.

Waziri Msaidizi wa Elimu Dkt Sara Ruto aliwapongeza wote walionufaika kati ya wote 11,000 waliotuma maombi kupata ufadhili huo.

Mwenyekiti wa JKF, Stella Samboja alisema wamewapa wanafunzi 148 ambao wamejiunga na kidato cha kwanza kote nchini.

  • Tags

You can share this post!

Waruguru aponda wawaniaji UDA

Redio za lugha mama zatakiwa ziwe na vipindi kuhusu jamii

T L