Joho na Sonko walimana ngumi kituo cha kura

Joho na Sonko walimana ngumi kituo cha kura

NA FARHIYA HUSSEIN

GAVANA wa Mombasa, Hassan Joho, na aliyekuwa gavana wa Nairobi, Mike Sonko (pichani), walizabana ngumi jana katika kituo cha kupigia kura kilicho eneobunge la Mvita.

Kisa hicho kilitokea katika kituo cha kura cha ukumbi wa Tudor Village ambapo awali kulikuwa kumetokea fujo zilizosababisha mgombeaji ubunge, Bw Omar Shallo, na Bw Samir Bhallo anayewania udiwani Tudor, kukamatwa na polisi.

Polisi walilazimika kuingilia kati kutawanya umati uliokuwa umeanza kushambuliana wakati Bw Joho na Bw Sonko walikuwa wakipigana.

Mkuu wa uchaguzi Mombasa, Bi Swalhah Yusuf alisema, kituo hicho kimevutia siasa tele kwa vile kina idadi kubwa ya wapigakura.

Bw Joho alikuwa ameandamana na mbunge anayeondoka wa Mvita, Bw Abdulswamad Nassir.

  • Tags

You can share this post!

Ufugaji farasi kwa ajili ya donge, starehe na michezo

Amerika yataka Afrika ikatae ‘kutumiwa vibaya’

T L